WAAMUZI KULINDWA ILI WASIPOKEE MLUNGULA AFCON 2013.
|
Mvuso Mbebe |
KAMATI ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 inatarajia kuwaweka faragha waamuzi wakati wa michuano hiyo itakayofanyika nchini Afrika Kusini ili kujaribu kuzuia tatizo la upangaji wa matokeo. Ofisa Mkuu wa kamati hiyo Mvuso Mbebe amesema kuwa waamuzi wa michuano hiyo watalindwa kwa kiwango sawa kama ilivyokuwa wakati michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ambayo nchi hiyo pia iliandaa. Mbebe amesema watatumia mbinu walizotumia katika michuano ya Kombe la Dunia ambao waliwaweka waamuzi wote katika hoteli ambayo hakuna raia yoyote aliyepata nafasi ya kuwaona na wakiondoka ni kw ajili ya kwenda kuchezesha mechi hivyo ni vigumu kwa watu kukutana nao na kuwarubuni. Watu wa Usalama watakuwa wakiwasindikiza waamuzi hao kutoka hotelini mpaka viwanjani na utaratibu huo utatumika toka mwanzo wa mashindano mpaka mwisho ambapo Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF limeridhia utaratibu huo. Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Januari 19 mpaka Februari 10 2013.
No comments:
Post a Comment