Friday, November 2, 2012

RONALDINHO ANUSURIKA KATIKA AJALI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil, Ronaldinho Gaucho amenusurika katika ajali ambayo ilihusisha magari matatu kugongana. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akiendesha gari lake kuelekea mazoezini wakati ajali hiyo inatokea lakini alikuwa na bahati kutoka katika jail hiyo bila kujeruhiwa lakini mmoja wa madereva alikimbizwa hospitali baada ya ajali hiyo. Magari yaliyohusika katika hiyo yaliumia vibaya lakini abiria waliokuwa katika moja ya gari ambalo lilikuwa ni basi walitoka salama bila majeraha yoyote. Mchezaji mwenzake aitwae Jo alipita katika eneo la ajali na kumchukua Ronadinho kuendelea na safari yake ya kuwenda mazoezini. Ronaldinho ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, amekuwa katika kiwango kizuri toka ahamie katika klabu hiyo akiwa ameshafunga mabao saba mpaka sasa na anatarajiwa kucheza katika mchezo wa Jumapili ambao Atletico itasafiri kuifuata Coritiba.

No comments:

Post a Comment