Thursday, November 15, 2012

SUAREZ NOT FOR SALE - RODGERS.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amesema uwa mshabuliaji nyota wa kikosi chake Luis Suarez atabakia klabuni hapo na kusisitiza kuwa hakuta kuwa na dau lolote la kuuzwa kwa mchezaji hyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Suarez mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia kwa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Manchester City hatahivyo Rodgers alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa nyota huyo atabakia klabuni hapo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alisaini mkataba mpya na Liverpool katika kipindi cha ajira ya kiangazi na amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu akiwa amefunga mabao 11 katika michezo 16 aliyocheza. Suarez alihamia Liverpool akitokea Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa ada ya paundi milioni 22.7 Januari mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment