Thursday, November 15, 2012
SANCHEZ NJE WIKI NNE.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Alexis Sanchez atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne baada ya kuumia mguu. Sanchez mwenye umri wa miaka 23 alilazimika kutolewa baada ya dakika 20 toka kuanza kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya nchi yake na Serbia Jumatano ambapo matokeo ya uchunguzi yamethibisha kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja kipindi hicho. Kama majeraha hayo yakimuweka nje ya uwanja kwa kipindi hicho kama Barcelona wanavyohofia inamaanisha kuwa nyota huyo atakosa michezo muhimu miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Spartak Moscow na Benfica pamoja na ule wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid. Sanchez amekuwa na historia ya kurejea katika majukumu ya kimataifa akiwa amjeruhi mara kwa mara kitu ambapo kimekuwa kikimnyima usingizi kocha wa Barcelona Tito Vilanova ambaye majeruhi katika kikosi chake kimekuwa kitu cha kawaida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment