Thursday, November 15, 2012
NAHODHA WA ZAMANI CAMEROON AFARIKI DUNIA.
SHIRIKISHO la Soka la Cameroon limesema kuwa aliyekuwa nahodha wa zamani wa Cameroon, Theophile Abega ambaye alikiongoza kikosi cha nchi hiyo kushinda taji lake la kwanza karibu miongo mitatu iliyopita amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58. Katika taarifa ya shirikisho hilo iliyotumwa katika mtandao haikufafanua haswa chanzo cha kifo cha nyota huyo lakini kuna taarifa zilizozagaa kwamba nyota amefariki dunia kutokana na tatizo la moyo wake kusimama ghafla inayojulikana kitaalamu kama Cardiac Arrest. Abega alikuwa nahodha wa Cameroon wakati iliponyakuwa kwa mara kwanza Kombe la Mataifa ya Afrika mwkaa 1984 wakati alipofunga bao katika ushindi wa mabao 3-1 iliyopata nchi hiyo dhidi ya Nigeria jijini Abidjan, Ivory Coast. Katika mwaka huo Abega ambaye pia alikuwa ya kikosi cha Cameroon kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1982, alitajwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kutokana na mchango wake alioonyesha katika michuano hiyo. Nyota hyo amewahi kucheza katika klabu ya Canon Younde katika miaka ya 80 kabla ya kutimkia Ulaya katika klabu ya Toulouse ya Ufaransa na baadae Vevey Sport ya Switzerland na baadae kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 33.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment