Thursday, November 15, 2012

WILSHERE ATOA TAHADHARI.

Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere amevionya vilabu vingine vya Ligi Kuu nchini Uingereza kwa kusisitiza kuwa bado hajapona kwa asilimia mia majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa miezi 17 kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu Wilshere alirejea tena katika kikosi cha Arsenal mwezi uliopita pamoja na kuitwa tena katika kikosi cha Uingereza katika mchezo dhidi ya Sweden ulochezwa Jumatano. Lakini pamoja na hayo Wilshere anaamini kuwa bado hajafikia kiwango chake kwa asilimia mia na bado hajafahamu ni lini atakuwa amepona kabisa kifundo chake cha mguu. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger na kocha wa Uingereza Roy Hodgson walijikuta katika mzozo juu ya afya ya Wilshere baada ya Hodgson kumjumuisha kiungo huyo katika kikosi chake kilichopambana na Sweden Jumatano.

No comments:

Post a Comment