Thursday, November 15, 2012

HATUNA FEDHA ZA KUMSAJILI ROBINHO - RAMALHO.

KOCHA wa klabu ya Santos, Muricy Ramalho amesema kuwa kumsajili Robinho kutahitaji uwekezaji mkubwa kitu ambacho klabu hiyo ya Brazil haiko katika nafasi ya kufanya hivyo. Robinho ambaye amewahi kucheza katika klabu za Real Madrid na Manchester City amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kurejea Santos ambayo ni klabu yake ya zamani akitokea AC Milan ya Italia lakini vikwazo vya kifedha linaonkana wazi kukwamisha suala hilo. Ramalho amesema kuwa kuna wachezaji wengi ambao walikuwa waawahitaji kuongeza nguvu katika kikosi chake lakini watakuwa mzigo mkubwa kiuchumi na Robinho ni mmoja wapo. Robinho mwenye umri wa miaka 28 ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Milan msimu huu akiwa ameonekana mara sita pekee katika mashindano yote ikiwa ni matokeo ya majeruhi ya mara kwa mara yanayomsumbua.

No comments:

Post a Comment