Thursday, November 15, 2012

SIJUTII KUIHAMA MACLAREN - HAMILTON.

DEREVA nyota wa Langalanga, Lewis Hamilton amekanusha taarifa za kiongozi wa timu ya MacLaren Martin Whitmarsh kuwa anajutia kitendo chake cha kuhamia timu ya Marcedes msimu ujao. Hamilton amesema kuwa ameshangazwa kidogo na kauli ya Whitmarsh aliyotoa wiki iliyopita kuhusiana na kuhama kwake na kusisitiza kuwa ulikuwa umuzi mgumu kuihama McLaren lakini kamwe hajajutia uamuzi huo. Marcedes walishinda mbio za Chinese Grand Prix April mwaka huu na kuonyesha kiwango kizuri mwanzoni mwa msimu baada ya kushindwa kutamba katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011 lakini wameonyesha kuporomoka tena katika kipindi hiki cha mwishoni mwa msimu. Hamilton ambaye alikuwa katika mbio za ubingwa wa dunia mwishoni mwa msimu huu ameshindwa kufanya hivyo baada ya gari lake kuharibika katika mashindano ya Abu Dhabi Grand Prix. Kushindwa kutamba katika mashindano hayo kumewapa nafasi wapinzani wake Sebastian Vettel wa Red Bull na Fernando Alonso wa Ferrari kubakia peke yao katika kugombea taji la dunia huku yakiwa yamebakia mashindano mawili kabla ya msimu kumalizika.

No comments:

Post a Comment