Wednesday, November 7, 2012

TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI MBILI FIFA.

TANZANIA imeporomoka tena kisoka kwa nafasi mbili mpaka nafasi ya 134 katika orodha ya viwango inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ya Octoba mwaka huu. Hispania imeendelea kushikilia usukani wa orodha hizo wakiwa katika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na nafasi ya tatu inashikiliwa na Argentina ambao wamepanda kwa nafasi moja wakiiporomosha Ureno mpaka nafasi ya nne. Italia imekwea mpaka nafasi ya tano ikichukua nafasi ya Uingereza walioangukia nafasi ya sita wakifuatiwa na Uholanzi ambao nao wamedondoka kwa nafasi moja, nafasi ya nane inashikiliwa na Colombia ikifuatiwa na Urusi huku kumi bora ikifungwa na Croatia. Kwa upande wa Afrika Ivory Coast imeendelea kuongoza wakiwa katika katika nafasi ya 15 duniani wakifuatiwa na Algeria ambao wako katika nafasi ya 19 wakati Mali na Ghana zinafuatana katika nafasi ya 28 na 29 na tano bora kwa upande wa Afrika inafungwa na mabingwa wa soka Afrika Zambia ambao wako katika nafasi ya 39. 

No comments:

Post a Comment