Monday, November 12, 2012

TERRY AMUWEKA DI MATTEO ROHO JUU.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Roberto Di Matteo ameonyesha kutishwa baada ya beki John Terry kuumia mguu wakati kikosi chake kilipotoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Liverpool katika Uwanja wa Stamford Bridge. Terry ndiye aliyefunga bao la kuongoza la Chelsea katika mchezo huo wa jana kabla ya kubebwa katika machela kufuatia kugongana kwa bahati mbaya na Luis Suarez ambaye alifunga bao la kusawazisha katika kipindi cha pili. Nahodha huyo wa Chelsea ambaye alikuwa anacheza kwa mara ya kwanza akitoka kwenye adhabu ya kufungiwa michezo minne kutokana na kukutwa na hatia ya ubaguzi wa rangi anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi baadae leo ili kuangalia ukumbwa wa tatizo lake. Di Matteo amesema kuwa anatarajia kuwa halitakuwa tatizo kubwa kwani bado wanamhitaji na alidhihirisha hilo kwa kiwango cha juu alichokionyesha kwenye mchezo huo kabla ya kutolewa baada ya kuumia. Kocha huyo pia amesema mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu hiyo Didier Drogba ataruhusiwa kufanya mazoezi katika makao makuu yaliyopo Cobham kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika Afrika Kusini, Januari mwakani.

No comments:

Post a Comment