Tuesday, November 13, 2012

DJOKOVIC BINGWA ATP WORLD TOUR.

MCHEZAJI nyota wa tenisi Novak Djokovic amefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa michuano ya ATP World Tour baada ya kumfunga Roger Federer katika mchezo wa fainali uliofanyika katika Uwanja wa O2 Arena jijini London Uingereza. Djokovic raia wa Serbia alimfumnga Federer raia wa Switzerland kwa 7-6 7-5 na kumaliza msimu akiwa katika nafasi ya kwanza kwenye orodha za ubora za mchezo huo pamoja na taji la michuano ya wazi ya Australia. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Djokovic ambaye hilo ni lake lake la pili la michuano ya ATP amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu lakini anashukuru alitulia na kuhakikisha ananyakuwa unshindi huo. Michuano ya ATP World Tour ndio michuano ya mwisho ya tenisi msimu huu mpaka Januari mwakani ambapo wataanza msimu kwa michuano ya wazi ya Australia.

No comments:

Post a Comment