Tuesday, November 13, 2012
MAANDALIZI YA AFCON 2013.
IVORY Coast ni mojawapo ya nchi 14 zilizofuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 ambazo zitaanza maandalizi yake kwa kucheza michezo ya kimataifa ya kirafiki sehemu mbalimbali duniani wiki hii. Ghana na Cape Verde zenyewe zitapimana nguvu jijini Lisbon, Ureno ikifuatiwa na Nigeria ambao watapimana nguvu na Venezuela jijini Miami, Marekani huku wenyeji Afrika Kusini watawakaribisha mabingwa wa Afrika Zambia jijini Johanneburg. Ivory Coast, Ghana, Cape Verde, Afrika Kusini, Angola, Morocco, Niger, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Zambia, Nigeria, Burkina Faso, Algeria, Tunisia na Togo ni timu zilizofuzu ambazo zote zitakuwa katika viwanja tofauti kucheza michezo ya kirafiki. Timu za Mali na Ethiopia ndio timu pekee kati ya 16 zitazoshiriki michuano ya ya Mataifa ya Afrika ambayo itaanza kutimua vumbi Januari 19 mpaka Februari 10 mwakani nchini Afrika Kusini ambazo hazitacheza michezo ya kirafiki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment