Tuesday, November 13, 2012

FALCAO ANAPASWA KULINDWA KAMA MESSI NA ROALDO - SIMEONE.

MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone anaamini kuwa waamuzi huwa wanatoa maamuzi tofauti kwa washambuliaji Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ukilinganisha mshambuliaji wa kikosi chake Radamel Falcao. Akihojiwa Simeone amesema huwa hapendi kuingilia maamuzi ambayo hutolewa na maamuzi lakini iko wazi kuwa Ronaldo na Messi wanaoguswa inakuwa ni adhabu tofauti na inavyotokea kwa nyota wake Falcao anapoguswa hakuna adhabu yoyote inayotolewa. Simeone ameshauri kuwa yota wake ana kiwango sawa na nyota hao hivyo waamuzi wanapaswa kumlinda kama wanavyowalinda Messi na Ronaldo. Atletic Madrid kwasasa wanashika nafasi ya pili nyuma ya Barcelona kwa alama tatu wakifuatiwa na Madrid ambao wanashika nafasi ya tatu huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 11 mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment