Thursday, November 8, 2012

TUNISIA KUWEKA KAMBI QATAR.

SHIRIKISHO la Soka nchini Tunisia limetangaza kuwa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitafanya maandalizi yake nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani Afrika Kusini. Tunisia inatarajiwa kuweka kambi ya siku 12 jijini Doha kwa ajili ya maandalizi hayo ambapo wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mali na Burkina Faso. Msafara wan chi hiyo unatarajiwa kutua katika mji wa Rustenburg, Afrika Kusini Januari 15 ambapo kundi D ambalo litakuwa na timu za Ivory Coast, Algeria na Togo ndio zitacheza michezo ya hatua ya makundi katika michuano hiyo. Kabla ya kuelekea Qatar chi hiyo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Switzerland Novemba 14 mwaka huu na kocha wa Sami Trabeslsi tayari ametangaza kikosi cha wachezaji 22 tayari kwa ajili ya mchezo huo.

No comments:

Post a Comment