Sunday, November 11, 2012

WALCOTT HATIHATI KUIKOSA SWEDEN - WENGER

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amebainisha kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo yuko katika hatihati ya kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu ya taiafa ya Uingereza na Sweden wiki ijayo kufuatia kuumia msuli katika mchezo wa Ligi Kuu ambao Arsenal ilitoka sare ya mabao 3-3 na Fulham. Mchezo huo uliochezwa jana ndio ulikuwa wa kwanza kwa Walcott kuanza toka ligi hiyo ilipofunguliwa ambapo mpira wa kona aliopiga mwanzoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo ulipelekea Olivier Giroud kuifungia Arsenal bao la kuongoza kwa kichwa. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Wenger amesema kuwa Walcott alikuwa na tatizo la misuli na alikaribia kumpumzisha wakati wa mapumziko wakati alipkaribia kuanguka lakini waliamua kumuacha baada ya kuona kama anaendelea vyema. Wenger aliendelea kusema kuwa katika dakika za mwishoni hali yake ilizidi kuwa mbaya hivyo kuamua kumpumzisha na hadhani kama ataweza kujumuika na wenzake katika kikosi cha Uingereza.

No comments:

Post a Comment