Sunday, November 11, 2012

BOATENG KUIKOSA UHOLANZI.

BEKI wa kimataifa wa Ujerumani, Jerome Boateng anatarajiwa kuukosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya nchi yake na Uholanzi mchezo ambao utachezwa Jumatano baada ya kupata majeraha kwenye kinena. Beki huyo alipata majeraha hayo wakati wa mchezo wa Bundesliga baina ya timu yake ya Bayern Munich na Eintracht Frunkfurt ambapo Bayern walishinda kwa mabao 2-0. Boateng mwenye umri wa miaka 24 alitolewa nje katika dakika ya 32 ya mchezo huo uliofanyika jijini Munich ambapo sasa anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili. Pamoja na maumivu hayo Boateng amefurahishwa na matokeo ambayo Bayern iliyapata katika mchezo huo ingawa kwa upande mwingine amesikitika kushindwa kuliwakilisha taifa lake katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uholanzi. Boateng anakuwa ni mchezaji wa pili kukosekana katika ukuta wa Ujerumani kwenye mchezo huo baada ya beki mwingine wa kati wa timu hiyo Holger Badstuber naye kuwa nje ya kikosi hicho kutokana na majeruhi.

No comments:

Post a Comment