Sunday, November 11, 2012

KLITSCHKO ATETEA MATAJI YAKE.

BONDIA nyota wa uzito wa juu duniani, Wladimir Klitschko amefanikiwa kutetea mataji yake ya IBF, IBO, WBO na WBA baada ya kumpiga Mariusz Wach kutoka Poland kwa pointi katika pambano lilifanyika jijini Humburg nchini Ujerumani. Katika pambano hilo Klitschko alionekana kushindwa kuonyesha kuonyesha cheche zake katika raundi tano za kwanza lakini baadae alionyesha kurudi mchezoni na kuanza kumshambulia makonde mfululizo mpinzani wake ambaye alionyesha kuchoka baada ya raundi ya tano. Waamuzi wa mchezo huo walitoa alama 120-107, 120-107 na 119-109 huku alama nyingi kati ya hizo zikimwendea Klitschko ambaye alifanikiwa kutetea mataji yake katika mapambano 13 aliyocheza. Hii ni mara ya kwanza kwa Klitschko kupambana bila kocha wake nguli wa mchezo huo Emanuel Steward ambaye alifariki mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 68 kwa ugonjwa wa kansa.

No comments:

Post a Comment