Sunday, November 11, 2012

NI VIGUMU KUCHEZA KWA KIWANGO KILA BAADA YA SIKU TATU - RIBERY.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery amekiri kuwa klabu yake inapata wakati mgumu kucheza kwa kiwango kutokana na kucheza mechi kila baada ya siku tatu pamoja na kuongoza Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu kama Budesliga kwa alama saba zaidi. Ribery aliifungia bao la kuongoza Bayern katika dakika ya 44 dhidi ya Eintracht Frankfurt kabla ya kiungo wa kimataifa wa Austria David Alaba kufunga bao la pili na kupelekea timu hiyo kuondoka kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa Allianz Arena jijini Munich. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ribery amekiri kuwa kucheza kila baada ya siku tatu sio kazi rahisi tofauti na wapinzani wao Frankfurt ambao wenyewe walikuwa wamepumzika kutokana na kutokuwa na mechi zingine zaidi ya ligi. Ribery mwenye umri wa miaka 29 ambaye alijiunga na Bayern mwaka 2009 aliendelea kusema kuwa ratiba ya mechi za Bundesliga, Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya ndio inachangia wawe wanacheza mechi kila baada ya siku tatu kitu wakati mwingine inakuw vigumu kucheza kwa kiwango walichokizoea. Pamoja na kauli yake hiyo kocha wa kikosi cha Ufaransa, Didier Deschamps amemjumuisha mchezaji huyo katika kikosi chake kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia mchezo ambao utafanyika jijini Parma Jumatano ijayo.

No comments:

Post a Comment