Monday, November 12, 2012

WENGER AMUWINDA DZEKO JANUARI.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amewaweka katika rada zake mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko baada ya kuruhusiwa kuongeza nguvu katika kikosi chake katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Viongozi wa klabu hiyo wameamua kumpa fedha Wenger kutokana na klabu hiyo kuonyesha kusuasua kukaa katika nafasi nne za juu za msimamo wa Ligi kuu nchini Uingereza kitu ambacho kinaweza kuwakosesha kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Kocha huyo raia wa Ufaransa ametaja nafasi tatu zinazopwaya katika kikosi chake ambazo ni nafasi ya mshambuliaji wa pembeni na kati pamoja na golikipa. Mbali na Wenger kumuwinda Dzeko ambaye hana furaha City baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza lakini pia anawamulika washambuliaji wengine kama Fernando Llorente anayecheza katika klabu ya Athletic Bilbao na Adrian Lopez wa Atletico Madrid. Wenger pia ammtengea kitita cha paundi milioni tisa winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 20 ingawa mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parish ameshatangaza kiasi cha paundi milioni 15 kwa klabu inayomhitaji mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment