Friday, December 14, 2012

ABRAMOVIC KUFANYA KUFURU KWA FALCAO.

MMILIKI wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovic anajiandaa kumfanya Radamel Falcao kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo kwa kumpatia mkataba ambao utamuwezesha kuchukua kitita cha paundi milioni 10 kwa mwaka. Chelsea inampa kipaumbele mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia ili iweze kumsajili katika dirisha dogo na bilionea wa Urusi anataka kuhakikisha nyota huyo anatua Stamford Bridge. Klabu hiyo inayotoka magharibi mwa jiji la London inatarajia kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mkataba mnono ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 200,000 kwa wiki. Malipo hayo ya Falcao yatakuwa yamepita yale anayolipwa Fernando Torres ambaye analipwa paundi 175,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment