Friday, December 14, 2012

LAMPARD AHOFIA CHELSEA KUMTEMA.

KIUNGO wa klabu ya Chelsea Frank Lampard anahofia muda wake kucheza soka katika klabu hiyo umekwisha katika kipindi hiki wakati mkataba wake umebakia miezi sita huku kukiwa hakuna mazungumzo yoyote mpaka hivi sasa. Lampard anataka kuongeza mkataba mwingine na klabu hiyo ambayo ameichezea kwa kipindi cha miaka 12 lakini inaonekana kama Chelsea hawahitaji huduma ya mchezaji huyo kwakuwa hakuna dalili zozote za kuanza mazungumzo juu ya mkataba mpya. Kiungo nyota tayari amehusishwa na taarifa za kwenda katika vilabu vya Los Angeles galaxy ya marekani, Paris Saint-Germain ya Ufaransa na vilabu vingine vya Urusi na China lakini akihojiwa jana usiku amesema kuwa angependa kubakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Lampard alijunga na Chelsea mwaka 2001 akitokea katika klabu ya West ham United kwa ada ya paundi milioni 11 na toka kipindi hicho amekuwa tegemeo na sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo inayotoka magharibi mwa jiji la London. 

No comments:

Post a Comment