Monday, December 10, 2012

ARSENAL YAMMENDEA NANI KATIKA DIRISHA DOGO.

KLABU ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kumnyakuwa winga wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Manchester United, Nani katika kipindi cha usajili wa dirisha januari mwakani. Nani mwenye umri wa miaka 26 yupo mguu nje mguu ndani Old Traford baada ya meneja wa United kushindwa kumuongeza mkataba na Wenger anataka kutumia nafasi hiyo ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Ligi Kuu nchini Uingereza. Winga huyo ambaye alikosa mchezo wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao Manchester City amekuwa akigombea namba na kiungo wa united anayechipukia Davide Petrucci mapema msimu huu. Wenger pia anapanga kumsajili kiungo wa kimataifa wa Senegal na klabu ya West ham United Mohamed Diame ambaye mkataba wake unatarajiwa kugharimu kiasi cha paundi milioni 3.5.

No comments:

Post a Comment