Monday, December 17, 2012

BARCELONA YAJIKITA ZAIDI KILELENI.

KLABU ya Barcelona imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya kuisambaratisha Atletico Madrid kwa mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa jana usiku. Ushindi huo unaifanya timu hiyo kuongoza La Liga kwa tofauti ya tisa dhidi ya Atletico ambao wanashika nafasi ya pili huku wakiwaacha wapinzani Real Madrid kwa alama 13 baada ya timu hiyo kupata sare ya kushangaza ya mabao 2-2 dhidi ya Espanyol jana. Barcelona mbao wananolewa na kocha Tito Vilanova ilibidi wapambane katika mchezo wa jana baada ya mshambuliaji nyota wa Atletico Radamel Falcao kuipa timu yake bao la kuongoza kabla yaAdriano kusawazisha bao hilo na Sergio Busquest akiongeza lingine huku mabao mengine mawili yakifungwana Messi. Barcelona sasa inaongoza La Liga ikiwa na alama 13 baada ya kucheza michezo 16 wakifuatiwa na Atletico wenye alama 37 huku mabingwa watetezi Madrid wakiwa katika nafasi ya tatu kwakuwa na alama 33.

No comments:

Post a Comment