Monday, December 17, 2012

BOLT ASHINDA TUZO YA BBC.

MWANARIADHA nyota wa mbio fupi Usain Bolt ameteuliwa kupewa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka kutoka nje tuzo ambayo imetolewa na BBC. Bolt mwenye umri wa miaka 26 raia wa Jamaica aling’ara katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London mwaka huu baada ya kufanikiwa kutetea medali zake mbili katika mbio za mita 100 na 200 pamoja na zile za kupokezana vijiti za mita 400. Mafanikio hayo aliyopata katika olimpiki yanamfanya kuwa mwanaridha pekee aliweza kutetea medali zake katika michuano ya olimpiki miwili tofauti. Mbali na hivyo Bolt pia anakuwa mwanariadha pekee kuwahi kutokea kwa kunyakuwa medali sita katika olimpiki huku hiyo ikiwa ni mara ya tatu kunyakuwa tuzo hiyo katika kipindi cha miaka mitano.

No comments:

Post a Comment