Sunday, December 30, 2012

DJOKOVIC ANYAKUWA TAJI LA MUBADALA.

MCHEZAJI tenisi nyota anayeshika namba moja duniani, Novak Djokovic ameanza msimu mpya wa michuano ya tenisi baada ya kumfunga Nicolas Almagro kwa 6-7 6-3 6-4 katika fainali ya mashindano ya maonyesho ya Mubadala iliyofanyika jijini Abu Dhabi. Djokovic ambaye alionyesha kiwango kizuri katika mchezo wa nusu fainali baada ya kumtoa David Ferrer anayeshika namba tano wakati Almagro ambaye aliziba nafasi ya Rafael Nadal aliyejitoa alimfunga Janko Tipsarevic. Akihojiwa mara baada ya ushindi huo Djokovic alifurahia kunyakuwa taji la michuano hiyo ya Abu Dhabi kwa mara nyingine na kuwasifu wapinzani wake aliokutana nao kwamba walimpa changamoto kubwa ambayo itamsaidia katika michuano iliyo mbele yake. Wachezaji wote wanne walioshirki michuano hiyo wanatarajiwa kuelekea nchini Australia kwa ajili ya michuano ya wazi itakayoanza Januari 14 jijini Melbourne huku Djokovic akiwa bingwa mtetezi.

No comments:

Post a Comment