Friday, December 28, 2012
YANGA KUONDOKA ALFAJIRI DESEMBA 30 KUELEKEA UTURUKI.
WACHEZAJI 27 wa klabu ya Yanga, wanatarajia kuondoka kesho kwenda Uturuki kwa kuweka kambi ya wiki mbili. Yanga itaondoka saa 10:30 alfajiri kwa ndege ya shirika la ndege la Uturuki na kufika Instambul Jumatatu saa 4:30 asubuhi kabla ya kwenda katika mji wa Antarya ambapo wataweka kambi yao. Ofisa Habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto, alisema maandalizi yote kwa ajili ya safari hiyo yamekamilika na timu hiyo itafikia katika Hotel ya Sueon Beach ambayo iko katika ufukwe wa bahari. Kizuguto alisema ikiwa nchini humo iatacheza michezo mitatu ya kirafiki ya kimataifa na timu ambazo zitatangazwa mara baada ya timu hiyo kufika nchini Uturuki. Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Ali Mustapha 'Bartez' Said Mohamed na Yusuf Abdul, Geofrey Taita, Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Stephano Mwasika, Kevin Yondan na Nadir Haroub 'Canavaro'. Wengine ni Twite Kabange, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza, George Banda, Jerry Tegete, David Luhende, Rehani Kibindu na Simon Msuva. Aliwataja viongozi wa benchi la ufundi kuwa ni Kocha Mkuu Ernest Brandts, kocha msaidizi Fred Minziro, kocha wa makipa Razack Siwa, daktari Sufian Juma, Ofisa Utawala Hafidh Salehe, Ofisa Habari Baraka Kizuguto na Mohamed Nyenye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji. Yanga imetumia zaidi ya sh. milioni 50 kwa ajili ya kugharamai kambi ya timu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment