Tuesday, December 25, 2012

EVERTON KUIKADIA RUFANI KADI NYEKUNDU YA GOBSON.

KLABU ya Everton imetangaza kuwa itakata rufani kufuatia kadi nyekundu aliyopewa nyota wake Darron Gibson katika mchezo ambao walishinda mabao 2-1 dhidi West Ham United. Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United alitolewa na mwamuzi Anthony Taylor aliyechezesha mchezo huo kwa kumchezea vibaya Mark Noble wa West Ham katika dakika za majeruhi. Mshambuliaji wa West Ham Carlton Cole naye alitolewa nje mapema kutokana na tukio kama hilo alilofanya kwa beki wa Everton Leighton Baines. Rufani hiyo hiyo kama ikifanikiwa itamaanisha kuwa Gibson ambaye ni raia wa Jamhuri ya Ireland ataweza kucheza katika mchezo dhidi ya Wigan Athletic utakaochezwa katika siku ya maboksi Desemba 26.

No comments:

Post a Comment