Tuesday, December 25, 2012

MASHABIKI ANAPASWA KUHESHIMU TIMU ZINGINE - LOEW.

KOCHA wa timu taifa ya Ujerumani, Joachim Loew amewataka mashabiki wa soka wan chi hiyo kuheshima viwango vya timu nyingine na kutotegemea makubwa kutoka kwa timu yao ya taifa. Katika mahojiano yake na wavuti wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB Loew amesema kuwa anaamini mashabiki wa soka nchini humo watakuwa wamepata somo kwa mwaka huu kuelekea katika mwaka mpya. Amesema timu ya taifa ya Hispania imekuwa ikifanya kazi ili ishinde vikombe kwa miaka mingi hivyo Ujerumani nayo anafikiri inaweza kufanya vizuri kama ikiheshimu wapinzani wake kwani sio wao pekee wenye ndoto za kunyakuwa vikombe. Kocha huyo alimalizia kuwa ni mapema mno kwa mashabiki wa nchi hiyo kuzungumzia michuano ya Kombe la Dunia 2014 itakayofanyika nchini Brazil hivi sasa badala kusaidia kuandaa timu bora ambayo italileta kombe hilo wakati ukifika.

No comments:

Post a Comment