Tuesday, December 25, 2012

CASILLAS IS A PRIDE OF MADRID - DEL BOSQUE.

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amedai kuwa nahodha wa Real Madrid Iker Casillas ni mchezaji wa kujivunia wa klabu hiyo. Casillas ambaye amecheza michezo 143 akiwa na timu ya taifa aliachwa katika kikosi cha kocha wa Madrid Jose Mourinho katika safari Malaga na badala yake nafasi ilichukuliwa na golikipa namba mbili Antonio Adan. Real Madrid ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga walifungwa katika mchezo dhidi ya Malaga mabao 3-2 lakini Del Bosque ambaye ana umri wa miaka 61 alimtetea Casillas na kudai kuwa bado ana uwezo. Del Bosque amedai kuwa Casillas ni mchezaji aliyeanza kucheza klabuni hapo toka akiwa na umri wa miaka na ameifanyia mengi klabu hiyo hivyo inatakiwa kujivunia mchezaji wa aina yake.

No comments:

Post a Comment