Wednesday, December 26, 2012

MICHU KUITWA HISPANIA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Swansea City Michu anatarajiwa kuitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Hispania mapema mwakani kufuatia kucheza katika kiwngo cha juu katika msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Kocha wa Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia, Vicente del Bosque anatarajia kumuita mchezaji katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uruguay Februari 26 mwakani mchezo ambao utafanyika jijini Doha, Qatar. Katika kikosi hicho Michu ataungana na Iago Aspas ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Celta Vigo na amekuwa akihusihwa na tetesi za kwenda Swansea. Michu amekuwa akionyesha kiwango cha juu kwa upachikaji mabao toka liponunuliwa kwa ada ya dola milioni 3.2 kutoka klabu ya Rayo Vallecano katika kipindi cha majira ya kiangazi ambapo kwasasa anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 18.

No comments:

Post a Comment