Wednesday, December 26, 2012

HODGSON ATAKA CHANGAMOTO YA MIKWAJU YA PENATI KATIKA MICHEZO YA KIRAFIKI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson anaamini kuwa changamoto ya mikwaju ya penati katika michezo ya kirafiki ambayo watatoa sare inaweza kuisadia timu hiyo kuondokana na jinamizi la kupoteza nafasi katika michuano mikubwa. Uingereza imekuwa mhanga mkubwa wa kutolewa katika michuano mikubwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati wakiwa wamepoteza mara sita kati ya saba mara mwisho ikiwa katika robo fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Italia iliyofanyika Juni mwaka huu. Wakiwa katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, Hodgson amesema kuwa katka mojawapo ya mechi za kirafiki watakazotoka sare atashauri wapinzani wake wamalize mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Amesema kwa kufanya hivyo kutawaongezea uzoefu zaidi wachezaji mbele ya mashabiki wengi kuliko kufanya hivyo wakiwa mazoezini peke yake. Mwaka 2013 Uingereza itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil na baadae dhidi ya Ireland kabla ya kucheza na Scotland katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment