Wednesday, December 26, 2012

MABAO YANGU SIO MUHIMU KAMA TIMU HAISHINDI - MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa mabao anayofunga hayatakuwa na maana yoyote kama timu yake itakuwa haiwezi kushinda`mechi zake. Mshambuliaji huyo amekuwa katika kiwango kizuri miezi 12 ambapo amefunga mabao 91 na kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller aliyefunga mabao 85 katika kipindi cha mwaka mmoja lakini nyota huyo amesema ushindi wa timu yake ndio wenye umuhimu kuliko rekodi binafsi. Messi ambaye yuko nchini kwao Argentina kwa mapumziko ya kipindi cha baridi katika La Liga amesema amefurahi kufunga mabao mengi na kuvunja rekodi lakini mwaka ungekuwa mzuri zaidi kama wangishinda mataji kwani siku zote amekuwa akisisitiza mabao hayani maana yoyote kama timu haishindi chochote. Messi ambaye pia mwaka huu alipata mtoto wake wa kwanza aitwae Thiago amesema ujio wa mtoto huyo umemfanya awe mtu mwenye furaha na kuwashukuru wapenzi wote wa soka wa Argentina ambao husafiri kwenda kumshangilia wakati akicheza.

No comments:

Post a Comment