Monday, December 3, 2012

FERGUSON AMTAKA MOURINHO KUVAA VIATU VYAKE OLD TRAFORD.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ameonyesha imani yake kuwa Jose Mourinho ndio meneja anayefaa kuchukua nafasi yake wakati atakapoondoka Old Traford. Ferguson mwenye umri wa miaka 70 amekuwa kocha wa United toka mwaka 1986 na bado hajaamua rasmi lini ataachia nafasi hiyo kwa ajili ya kustaafu lakini alimsifia Mourinho ambaye anaifundisha Real Madrid kuwa kocha mwenye viwango vya kuingoza United katika siku za mbeleni. Kocha huyo amesema kuwa hakutegemea mtu ambaye hajawahi kucheza soka kama anaweza kuwa kocha bora lakini Mourinho mwenye umri wa miaka 39 amebadilisha dhana hiyo na anaweza kufundisha popote na kwa kiwango cha juu kabisa. Ferguson anakumbuka wakati Mourinho anaingia Uingereza na kujiita yeye wa kipekee na kuwaambia wachezaji wa Chelsea watashinda taji la Ligi Kuu nchini humo alimuona kama mwehu lakini alipoanza kazi alithibitisha usemi wake.

No comments:

Post a Comment