Monday, December 3, 2012

BUSQUETS AWASIHI WENZAKE KUTOBWETEKA.

KIUNGO nyota wa klabu ya Barcelona, Sergio Busquets amesisitiza kuwa hawatakiwi kujibweteka kama wanataka kushinda taji la Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga msimu huu. Barcelona wametofautia alama sita na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili kufuatia ushindi wa mabao 5-1 waliopata kutoka kwa Athletic Bilbao wakati bado wameacha pengo la alama 11 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid ambao wanashika nafasi ya tatu. Busquests aliiambia wavuti ya klabu hiyo kuwa pamoja na kuongoza La Liga kwa tofauti ya alama nyingi lakini safari bado ni ndefu kufikia mwishoni mwa msimu hivyo bado hakuna muda wa kupumzika kwa sasa. Kiungo huyo alimsifu mchezaji mwenzake nyota Lionel Messi na kudai kuwa ndio mchezaji bora wa dunia kwasasa kwasababu anaweza kufunga mabao na kuwa sehemu ya mashambulizi yote ambayo klabu imekuwa ikifanya. Messi alifunga mabai mawili katika mchezo dhidi ya Bilbao uliochezwa Jumamosi na kufikisha mabao 21 katika mechi 14 alizocheza msimu huu.

No comments:

Post a Comment