Monday, December 3, 2012

ABRAMOVICH KUMUITA GRANT ILI KUMUONGEZEA NGUVU BANITEZ.

MMILIKI wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anafikiria kuchukua hatua ya kushangaza ambayo itashuhudia kocha wa zamani wa klabu hiyo Avram Grant akirejea Stamford Bridge. Abramovic ambaye ni raia ya Urusi anahofia kuwa alifanya makosa kumleta Rafa Banitez kuinoa klabu hiyo na anaona kuna umuhimu wa kumuita tena Grant ili awe mshauri wa Banitez ili kutatua tatizo la klabu hiyo kuboronga. Toka Banitez apewe mikoba ya kuinoa klabu hiyo katika michezo mitatu iliyopita ameshindwa kubata ushindi na amekuwa akipata upinzani mkali kutoka kwa mashabiki ambao hawakufurahishwa na uteuzi wake. Baada ya kipigo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa West Ham United Jumamosi, Abramovic alizungumza na viongozi wa klabu hiyo kuangalia uwezekano wa kumleta Grant ambaye alimtimua mwaka 2008 baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ili amsaidie Banitez. Grant ambaye ni raia wa Israel amekuwa hana kibarua chochote toka alipoacha kuifundisha klabu ya Partizan Belgrade mwishoni mwa msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment