Monday, December 3, 2012

ADEBAYOR AJIENGUA KUSHIRIKI MATAIFA YA AFRIKA.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor amempa ahueni kocha wake Andre Villas-Boas baada ya kujiondoa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo inatarajiwa kufanyika Januari mwakani. Adebayor mwenye umri wa miaka 28 alitishia kujitoa katika timu ya taifa ya Togo kama wachezaji ahwatalipwa fedha ambazo walikuwa wakidai katika Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Akihojiwa nyota huyo amesema kuwa kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote atastaafu rasmi soka la kimataifa na wachezaji wengi wataacha kuichezea nchi yao. Kufuatia shirikisho la nchi hiyo kushindwa kutatu suala hilo mshambuliaji huyo ambaye amewahi kucheza katika klabu za Arsenal na Manchester City aliamua kujiondoa kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini ili kuonyesha msisitizo wa nia yake.

No comments:

Post a Comment