Monday, December 3, 2012

MARIGA AREJEA UWANJANI.

KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, Mcdonald Mariga ameshindwa kuzuia kuonyesha furaha yake wakati aliporejea tena uwanjani wakati Inter Milan ikishinda bao 1-0 dhidi ya Palermo Jumapili Jioni. Mariga amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi nane baada ya kuwa majeruhi na kudai kuwa kilikuwa kipindi kigumu mno lakini anashukuru amepona na amerejea tena kuitumikia klabu yake ya Inter. Kocha wa Inter, Andrea Stramaccioni alimpanga Mariga katika kikosi chake ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu kwa mkenya huyo kucheza mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A. Pamoja na kushindwa kufunga katika mchezo huo Mariga alionyesha kufurahishwa kurejea tena uwanjani na kuahidi kufanya vizuri zaidi huko mbeleni kama atapewa nafasi ya kucheza mara nyingi zaidi. Mariga alitengeneza historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati huo Jose Mourinho ambaye ni kocha Real Madrid ya Hipsnia kwasasa alipokuwa akiifundisha Inter Milan. 

No comments:

Post a Comment