Wednesday, December 26, 2012

FOMENKO KOCHA MPYA UKRAINE.

SHIRIKISHO la Soka nchini Ukraine-FFU limemtaja kocha Mikhail Fomenko kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Nafasi hiyo ambayo iliachwa wazi toka Septemba mwaka huu baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Oleg Blokhin kuondoka na kwenda kuifundisha klabu ya Dynamo Kiev baada ya michuano ya Ulaya kumalizika. Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester Ciy, Sven-Goran Eriksson ndio alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa kocha wan chi hiyo lakini mwishoni Fomenko ndio amethibitishwa kuchukua nafasi hiyo. Fomenko aliwashukuru maofisa FFU kwa kumwamini kumpa kibarua hicho na kwamba anatambua jukumu lake na changamoto zinazoikabili timu ya taifa ya nchi hiyo ambapo kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha wanafuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs aliwahi kukiri kuitaka nafasi hiyo kabla ya kukubali kuinoa Queens Park Rangers wakati mshambuliaji nyota wa zamani wa nchi hiyo Andriy Shevchenko alikataa nafasi ya kuifundisha nchi yake.

No comments:

Post a Comment