Wednesday, December 26, 2012

ODIMWINGIE AMALIZIA HASIRA ZAKE KWA IKPEBA.

Ikpeba
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya West Bromwich Albion, Peter Odemwingie kwa mara nyingine tena ametumia mtandao wa kijamii wa twitter kuonyesha hasira zake kufuatiwa kutemwa katika kikosi cha wachezaji 32 wa nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2013. Odemwingie alitumia mtandao huo kuwashambulia kocha wa Nigeria Stephen Keshi maofisa wa Shirikisho la Soka nchini Nigeria-NFF na mchezaji bora wa zamani wa Afrika Victor Ikpeba. Ikpeba alimtupia madongo Odimwingie katika kipindi cha Monday Night Football kinachorushwa hewani na Supersport akidai kuwa nyota huyo hajafikia mafanikio aliyofikia yeye Ikpeba. Odimwingie alijibu dongo hilo katika mtandao wa kijamii kwa kumponda Ikpeba na kudai kuwa alikuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria ambacho kilishindwa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika iliyofanyika mapema mwaka huu nchini Gabon na Equatorial Guinea.

No comments:

Post a Comment