Friday, December 28, 2012

HAKUNA KILICHOBADILIKA - CAVANI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya Napoli ya nchini Italia, Edinson Cavani amesisitiza kuwa hakuna chochote kilichobadilika baada ya kugundua kuwa klabu yake hiyo ilikataa ofa ya euro milioni 55 ili wamuuze. Cavani ndiye mshambuliaji ghali zaidi katika Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A akiwa amefunga mabao 13 katika ligi bao moja nyumba Stephan El Shaarawy ambaye anaongoza kwa ufungaji kwasasa. Dau hilo kubwa ambalo lilitolewa na klabu ambayo haijajulikana halijamuathiri nyota huyo ambaye amsisitiza bidii zake katika mazoezi ndizo zilizomfanya kufikia thamani hiyo. Cavani amesema taarifa za Napoli kukataa dau hilo haziwezi kumwathiri kwani amepanga kuendelea kuisaidia klabu hiyo katika mwaka 2013 kwa bidii zote ili waweze kupata mafanikio katika kila mashindano. Napoli inashika nafasi ya sita ikiwa nyuma ya klabu za Juventus, Fiorentina, Lazio na Inter Milan katika msimamo wa Serie A. 

No comments:

Post a Comment