Sunday, December 16, 2012

KHAN AMCHAPA MOLINA.

BONDIA machachari kutoka Uingereza, Amir Khan amefanikiwa kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Carlos Molina baada ya kupoteza mapambano mawili yaliyopita katika pambano lililofanyika jijini Los Angeles, Marekani. Khan mwenye umri wa miaka 26 alipoteza mikanda yake ya WBA na IBF ya uzito mwepesi baada ya kukubali kipigi kutoka kwa Danny Garcia na Lamont Peterson lakini bondia huyo alionekana kuimarika kiwango chake katika pambano dhidi ya Molina ambalo alimlazimisha mpinzani wake huyo kushindwa kuendelea katika raundi ya 10. Bondia huyo aliyekulia jijini Bolton aliwasili katika ukumbi wa Memorial Sports Arena huku akiwa na kumbukumbu ya kupigwa na Garcia ambaye alimgaragaza chini mara tatu katika raundi ya nne ya pambano lao lililofanyika Julai mwaka huu. Kwa ushindi aliopata katika pambano hilo Khan sasa anaweza kuamua kutafuta pambano la maruadiano kati ya Garcia au Peterson.

No comments:

Post a Comment