Sunday, December 16, 2012

SITAFANYA MANUNUZI JANUARI - FERGUSON.

MENEJA wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema hatafanya manunuzi yoyote ya mchezaji katika kipindi cha dirisha dogo la usajili baada ya timu yake kupata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland. Ushindi huo ambao ulitokana na mabao yaliyofungwa na Robin van Persie, Tom Cleverley na Wayne Rooney umeifanya timu hiyo kubakia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya alama sita na mahasimu wao Manchester City ambao wanashika nafasi ya pili. Pia ina maana kuwa United imefanikiwa kushinda mechi zake tano za ligi zilizopita rekodi ambayo inamfanya Ferguson kutohitaji mchezaji mwingine wa kuongeza nguvu katika kipindi cha dirisha dogo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ferguson ambaye amekuwa akihusishwa na tetesi za kumhitaji winga wa Arsenal Theo Walcott alikanusha taarifa hizo na kudai kuwa kikosi chake kina wachezaji wa kutosha ambao wanaweza kuhakikisha wananyakuwa taji la Ligi Kuu msimu huu.

No comments:

Post a Comment