Sunday, December 16, 2012

WEST HAM KUIPA WAKATI MGUMU ARSENAL KWA KUMUONGEZA MSHAHARA DIAME.

KLABU ya West Ham United inajipanga kumuongeza mshahara mara mbili ya kiwango anachopata hivi sasa kiungo wake Mohamed Diame ili kuizuia Arsenal kumchukua mchezaji huyo katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwaka huu. Kiungo huyo alijiunga na West Ham kama mchezaji huru akitokea Wigan Athletic katika kipindi cha majira ya kiangazi na amekuwa akionyesha kiwango bora toka atue katika klabu hiyo mpaka kuifanya Arsenal ianze kumnyatia. Diame ambaye ni raia wa Senegal anakadiriwa kuwa thamani ya paundi milioni 4.5 lakini maofisa wa West Ham wanajiamini kumbakisha mchezaji huyo kwa kumpa mshahara wa paundi 75,000 ambapo watasababisha na thamani ya mchezaji huyo kupanda pia. Klabu za Newcastle United, Fulham na Liverpool nazo pia zimeonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 lakini Arsenal ndio wenye uhitaji zaidi wa kiungo katika safu yake baada ya Abou Diaby kukaa nje kutokana na majeruhi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment