Sunday, December 16, 2012

WILSHERE KUONGEZA MKATABA ARSENAL.

KIUNGO Jack Wilshere anatarajia kuipa ahueni klabu yake ya Arsenal pamoja na meneja Arsene Wenger aliyekalia kuti kavu kwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano ambao una thamani ya paundi milioni 20. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 20, aliapa kuwa kizazi kipya cha wachezaji wa Arsenal kitaleta furaha katika klabu hiyo ambayo sasa imefikisha miaka saba na nusu bila kunyakuwa taji lolote. Wilshere ambaye anatarajia kukubali kusaini mkataba mpya hivi karibuni ikiwemo mshahara unaoanzia paundi 80,000 kwa wiki pia alibainisha nia yake ya kuja kuwa nahodha wa klabu hiyo katika siku za usoni. Mbali na Wilshere lakini pia winga Alex Oxlade-Chamberlain aye anatarajiwa kusaini mkataba mpya hivyo habari hizo kuwapoza mashabiki wa klabu hiyo ambao wiki iliyopita walishuhudia klabu yao ikitolewa katika Kombela Ligi na Bradford City.

No comments:

Post a Comment