Sunday, December 16, 2012

MESSI KUSAINI MKATABA MNONO BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi anatarajia kusaini mkataba wa maisha na klabu hiyo ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi kuliko mchezaji yoyote wa ligi kubwa barani Ulaya. Baba wa nyota huyo, Jorge tayari amekwishaanza mazungumzo na klabu hiyo kuhusu suala la kuongeza mkataba wa sasa na hiyo inamaanisha kuwa Messi atabakia Barcelona mpaka atapofikisha umri wa miaka 31. Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amepanga kumuongeza mkataba wa miaka miwili mchezaji huyo ili kuhakikisha anabakia klabuni hapo kabla ya kumpa mkataba mrefu nyota huyo wa Argentina kabla hajastaafu wadhifa huo. Messi kwasasa anachukua kitita kabla ya posho paundi milioni tisa kwa mwaka akiwa nyumba ya mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic anayechukua paundi milioni 12 kwa mwaka na Samuel Eto’o ambaye anachukua kitita paundi milioni 16 kwa mwaka akiwa na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.

No comments:

Post a Comment