Wednesday, December 19, 2012

MESSI ANASTAHILI BALLON D'OR - IBRAHIMOVIC.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSV, Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa Lionel Messi anastahili tuzo ya Ballon d’Or pamoja na kwamba mshambuliaji huyo wa Barcelona ameshashinda tuzo hiyo mara tatu mfululizo. Akihojiwa na gazeti moja nchini Ufaransa Ibrahimovic alimsifu Messi na kumfananisha kama mchezaji wa kwenye michezo ya luninga inayojulikana kama PlayStation na kudai kuwa anayeponda uwezo wa mchezaji huyo hajui mchezo wa soka. Ibrahimovic pia alisifu uwezo kiungo nyota wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa ni wa kipekee kwani pindi anapoingia uwanjani wachezaji wenzake wote hubadilika na kucheza vyema na kupelekea timu yao kupata matokeo mazuri. Nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alifika mbali na kudai kuwa hadhani kama kutatokea mchezaji wa aina ya Zidane huko mbele katika ulimwengu wa soka. 

No comments:

Post a Comment