Wednesday, December 19, 2012

TANZANIA YAPAA VIWANGO FIFA.

TANZANIA imekwea kwa nafasi nne mpaka nafasi ya 130 katika viwango vya ubora duniani vinavyotolewa leo na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA ambavyo ndio vitakuwa vya mwisho kwa mwaka 2012 huku ikishika nafasi ya 38 kwa upande wa Afrika. Katika orodha hizo Ivory Coast imeendelea kuongoza kwa upande wa Afrika kwa kukupanda nafasi moja mpaka nafasi ya 14 ikifuatiwa na Algeria waliopo katika nafasi ya 19 huku Mali wakiwa katika nafasi ya 25 baada ya kupanda kwa nafasi tatu. Nafasi ya nne kwa Afrika inashikwa na Ghana ambao wameporomoka kwa nafasi moja mpaka nafasi ya 30 wakifuatiwa na mabingwa wa Afrika Zambia ambao ndio wanafunga orodha ya tano bora, ambapo wamepanda nafasi nne mpaka nafasi ya 34. Kwa upande wa tano bora duniani Hispania bado wako katika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Ujerumani katika nafasi ya pili na Argentina nafasi ya tatu wakati nafasi ya nne inashikiliwa na Italia ambao wamepanda nafasi moja tofauti na mwezi uliopita. Nafasi ya tano katika orodha hizo inashikiliwa na Colombia ambao wamekwea kwa nafasi tano toka nafasi ya 10 waliyokuwepo mwezi uliopita huku mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil nao wakizidi kuporomoka mpaka nafasi ya 18 kutoka nafasi ya 13 walioyokuwepo mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment