Friday, December 14, 2012

NAPAMBANA ILI NIREJEE TENA UWANJANI - ABIDAL.

BEKI wa klabu ya Barcelona, Eric Abidal amesema kuwa atapambana kuhakikisha anarejea uwanjani tena wakati huu akiendelea kupona taratibu baada ya kubadilisha ini. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa aligundulika kuwa na uvimbe katika ini lake mwishoni mwa mwaka 2011 na alifanyiwa uapsuaji mkubwa wa kupandikizwa ini jingine machi mwaka huu na toka kipindi hicho amekuwa akipambana ili kurejea katika afya yake ya kawaida. Abidal amesema madaktari wamemwambia kuwa sio kawaida kwa watu wenye matatizo kama yake kuendelea kuishi hivyo atapambana ili aweze kucheza soka tena lakini kama itashindikana haitakuwa na tatizo atabakia na familia yake. Nyota huyo alitoa kauli hiyo wakati akipokea tuzo ya Prix Pyrenees kwa juhudi zake katika kupambana na maradhi ambayo yalikuwa yakimsumbua ambapo aliwashukuru wote waliokuwa pamoja naye katika mwaka huu ambao anadai ulikuwa mgumu zaidi katika maisha yake.

No comments:

Post a Comment