Friday, December 14, 2012
SERBIA YAPIGWA FAINI YA PAUNDI 80,000.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limeitoza faini Serbia ya paundi 80,000 na kucheza mchezo wao unafuata wa vijana chini ya miaka 21 milango ikiwa imefungwa kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya dhidi ya Uingereza Octoba mwaka huu. Mbali na adhabu hiyo lakini pia maofisa wawili wa benchi la ufundi na wachezaji wanne walifungiwa wakati wachezaji wawili wa Uingereza nao pia walifungiwa. Maofisa hao waliofungiwa ni kocha wa viungo Andreja milunovic na kocha msaidizi Predrag Katic ambao wote wamefungiwa miaka miwili kujishughulisha na masuala yoyote ya soka wakati wachezaji waliofungiwa ni Goran Causic mechi nne, Ognjen Mudrinski mechi tatu, Filip Malbasic mechi tatu na Nikola Ninkovic mechi mbili. Wachezaji wa Uingereza waliofungiwa ni pamoja na Steven Caulker mechi mbili na Thomas Ince mechi moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment