Sunday, December 9, 2012
PACQUIAO APIGWA KWA KNOCK OUT NA MARQUEZ.
BONDIA Juan Manuel Marquez amefanikiwa kumpiga kwa knock out katika raundi ya sita bondia machachari kutoka Philipines Manny Pacquiao katika pambano la uzito wa welter lililofanyika jijini Las Vegas, Marekani. Marquez raia wa Mexico mwenye umri wa miaka 39 alimgaraza Pacquiao ambaye alilala chini bila kujitambua kwa kidogo na kupata ushindi wake wa kwanza toka kwa bondia huyo katika mapambano manne ambayo wamekutana. Pacquiao mwenye umri wa miaka 33 ameshinda mapambano mawili huku moja wakitoka sare huku hilo likiwa pambano la pili mfululizo kwa bondia huyo kuchapwa baada ya kupoteza pambano lililokuwa na utata na bondia Timothy Bradley Juni mwaka huu. Kabla ya kuangushwa katika raundi ya sita Pacquiao alikuwa tayari amedondoshwa katika raudi ya tatu lakini alimudu kuamka na kuendelea na pambano hilo ambapo mpinzani Marquez alionekana akiwa amepania kuibuka mshindi. Pacquiao amesema kuwa lilikuwa pambano zuri na tayari aliona amemmudu mpinzani wake hivyo akaanza kujiamini ndio maana Marquez akatumia nafasi hiyo na kumpiga ngumi ambayo hakuitegemea na kushindwa kunyanyuka katika raundi ya sita. Pamoja na kupoteza mchezo huo Pacquiao amesema anataka kurudiana kwa mara nyingine tena bondia huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment